Na Kitengo cha Mawasiliano
Wananchi Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba wamesema wapo tayari kuhesabiwa Sensa ya Watu na Makazi Agosti 23,2022
Wamezungumza hayo Agosti 13,2022 baada ya ziara ya utoaji elimu na hamasa ya kushiriki zoezi la Sensa ambalo limefanyika katika kata zote 32 na Kamati ya Sensa Wilaya
Katika ziara hiyo timu husika za Wilaya zilianza kufanya kikao na kutoa elimu na hamasa kwa kamati za vitongoji,vijiji na kata ili ziweze kuendelea na uhamasishaji huo kila siku katika maeneo yao
Naye Mkuu wa Wilaya Mke.Kanali Patrick Sawala alitoa wito kwa viongozi wa vitongoji kutoa ushirikiano kwa makarani ambao watafika katika maeneo yao ili kuweza kudodosa
"Makarani watafika katika maeneo yenu kuanzia Agosti 21,2022 ambapo wataanza kuhoji dodoso la jamii kwa siku mbili kisha wataendelea na dodoso kuu Agosti 23,2022 muwape ushirikiano ili kukamilisha zoezi hili kwa asilimia mia moja,"amesema Dc Sawala
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa