Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Michael Mtenjele ameendelea na ziara yake akikagua Miradi ya Maendeleo katika Wilaya hiyo na kufika katika Mradi wa Maji Mitondi Kata ya Kitama unaotekelezwa na RUWASA na kuwapongeza kwa hatua ya utekelezaji waliyofikia.
Awali akisoma taarifa ya Mradi huo Meneja wa RUWASA Wilaya ya Tandahimba Mhandisi Antidius Muchunguzi amesema mradi umefikia 65% na utaghalimu Tsh. Milioni 792.2 ambapo Wananchi 4,025 katika Vijiji 7 watapata maji safi na Salama.
Aidha, Mhandisi Muchunguzi ameongeza kuwa katika utekelezaji wa mradi huo makundi mbalimbali yamenufaika ambapo jumla ya ajira 98 za mda mfupi zimetolewa ikiwemo Madereva, mama lishe na Mafundi Ujenzi.
Katika hatua nyingine Kanali Mtenjele ametembelea na kukagua Miradi mingine ikiwemo Vyumba vya Madarasa Shule ya Msingi Litehu, Ujenzi wa Bweni Luagala Sekondari, Mradi wa Bwawa la Ufugaji Viumbe maji Chaume, pamoja na Kituo Cha Afya Kitama.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa