Na Kitengo cha Mawasiliano
Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba imepata washiriki 80 katika fainali ya mashindano ya umitashumta kati ya washiriki 391 ambao watashiriki katika mashindano ngazi ya Mkoa
Timu ya mpira wa pete ikiwa inaendelea na mechi
Mashindano hayo yamefanyika Julai 9,2022 katika viwanja vya shule ya msingi Amani kata ya Tandahimba ambapo klasta sita ziliweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya fainali hiyo
Katika mashindano hayo michezo mbalimbali ilishindaniwa kama vile mpira wa mguu,mpira wa mkono,mpira wa kikapu,mpira wa pete,riadha,kuruka chini,kuruka juu, na kwaya ambapo mshindi wa jumla kwa michezo yote ni Klasta ya Mihambwe
Klasta ya mihambwe wakikabidhiwa kombe la msindi wa Jumla
Akifunga mashindano hayo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji,Afisa Taaluma Msingi ndg.Abdul Masudi amewataka washiriki hao kuongeza juhudi ili waweze kufikia lengo la kuwa washindi kuanzia ngazi ya Mkoa hadi Taifa
Aidha naye Mratibu Michezo Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba ndg.Omary Amlima amesema katika mashindano hayo washiriki 391walikaa kambi ambapo wavulana 186 na Wasichana 205
Amesema kuwa washiriki hao wanatarajiwa kuelekea katika mashindano ya Kimkoa na baadaye Kitaifa ambapo mwaka huu mashindano ya Umitashumta yatafanyika Mkoani Tabora
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa