Na Kitengo cha Mawasiliano
Walimu Wakuu na Walimu wa madarasa ya awali Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba wamepewa mafunzo ya kuwajengea uwezo kwa kuwaongezea maarifa na ujuzi kuhusu matumizi ya njia na vifaa vilivyoboreshwa vya mtaala wa Elimu kupitia mradi wa BOOST .
Akifungua mafunzo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Kaimu Afisa Elimu Awali na Msingi Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Mwl. Rajabu Saidi amewasistiza kuzing.atia mafunzo hayo ili yaweze kuinua taaluma na kuwawezesha wanafunzi wa awali kufahamu kusoma, kuhesabu na kuandika.
Kwa upande wake mratibu wa mafunzo hayo Mwl..Vitalis Chinguile amesema mafunzo hayo ya siku nne yamewakusanya walimu 120 wa shule za awali na msingi ambapo yatahitimishwa Januarii 12,2025.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa