Na Kitengo cha Mawasiliano
Walimu wa shule za Msingi za Serikali Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba wamepongezwa kwa kuongeza ufaulu kwenye matokeo ya Mtihani wa Taifa wa darasa la saba Mwaka 2023.
Hafla ya kuwapongeza walimu imeandaliwa na Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba kupitia Idara ya Elimu Msingi ambapo katika Klasta tano zilizopo Halmashauri ya Tandahimba kila klasta imefanya hafla hiyo katika eneo lake.
Aidha Mkuu wa Idara ya Elimu Awali na Msingi Mwl.Samweli Mshana amesema walimu kwa juhudi wamechangia kuongeza ufaulu wa darasa la saba na kufikia asilimia 85.2 mwaka 2023 na kushika nafasi ya 3 Kimkoa kati ya Halmashauri tisa kwa upande wa Mtihani wa Upimaji wa darasa la nne Mwaka 2023 Halmashauri ya Tandahimba imeshika nafasi ya kwanza Kimkoa kwa kupata asilimia 93 kati ya Halmashauri tisa za Mkoa wa Mtwara.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya Ndg.Francis Mkuti akizungumza kwenye hafla ya Klasta ya Matogoro Februari 22,2024 amewapongeza Walimu kwa juhudi zao na amewasistiza kuongeza juhudi hizo ili ufaulu uongezeke zaidi mwaka 2024.
Naye Mkuu wa Idara ya Rasilimaliwatu na Utawala Ndugu.Joshua Mgoli amewapongeza walimu lakini pia ametumia nafasi hiyo kuwakumbisha kuzingatia taratibu za uhamisho mara wanapojitaji kuhama ili kuepuka uhamisho feki ambao ni kosa kisheria.
Katika hafla ya Klasta ya Matogoro na Klasta ya Mihambwe zilihitimishwa kwa kukabidhi zawadi mbalimbali vikiwemo vyeti vya pongezi na fedha taslimu kwa walimu waliofanya vizuri katika masomo yao wanayoyafundisha .
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa