Na Kitengo cha Mawasiliano
Walengwa wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii(TASAF)Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba wamepewa elimu ya umuhimu wa kushiriki sensa ya watu na makazi kwa ajili ya maendeleo ya vijiji vyao na Taifa kwa ujumla
Elimu hiyo imetolewa na wawezeshaji wakati wa uhaulishaji wa ruzuku kwa walengwa wa kaya maskini ambapo walitumia nafasi hiyo kabla ya kuanza malipo kutoa elimu kuhusu sensa ya watu na makazi
Akizungumza na walengwa leo Julai 29,2022 wawezeshaji wa kijiji cha Nanjanga kilichopo kata ya Ngunja ndugu. Karim Aibu amesema kuwa lengo la Serikali ni kupata takwimu sahihi itakayosaidia kupanga mipango ya maendeleo
“Sensa ya Watu na makazi italeta maendeleo katika vijiji vyetu ni muhimu kuhudhuria,msiwe na Imani potofu ya kutoshiriki na msikubali mtu awapotoshe kuhusu sensa,lengo la serikali ni njema katika kuleta maendeleo kwa wananchi wake,”amesema Mwezeshaji
Mwezeshai Ndg Silas Kibaya akimkabidhi Mlengwa malipo yake
Aidha kiasi cha shilingi 259,329,895 zimetumika kuahulishwa kwa walengwa wa taslimu 9473 katika vijiji 157 ikiwa ni malipo ya mwezi Mei na June,2022 ambapo zoezi hilo la siku nne limekamilika leo Julai 29,2022
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa