Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Wakuu wa Idara na Vitengo Halmashauri ya Tandahimba wametembelea miradi inayotekelezwa na Halmashauri yenye thamani zaidi ya milioni 566 ambazo zimetokana na fedha za mapato ya ndani ,Serikali kuu na Tea kwa mwaka 2019/2020 ili kuweza kujionea hatua mbalimbali ya miradi hiyo ilipofikia
Katika Ziara hiyo miradi zaidi ya 42 kati ya miradi 72 inayotekelezwa imeweza kufikiwa na wakuu wa idara na vitengo
Kaimu Mkurugenzi Ally Machela akitoa maelekezo
Baadhi ya miradi iliyofikia hatua ya kumalizika ni pamoja na vyumba vya madarasa ,baadhi ya matundu ya vyoo, Zahanati na miradi mingine ipo katika hatua ya mwisho huku mingine ikiendelea katika hatua mbalimbali
Zahanati ya Mambamba ipo katika hatua za mwisho
Akizungumza mara baada ya kumaliza kutembelea kata 17 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Tandahimba Ally Machela amesema hiyo ni awamu ya kwanza ,awamu ya pili watatembelea miradi iliyobaki ili kila mmoja awe anaijua miradi yote iliyopo
Wakuu wa Idara na vitengo walitembelea Ujenzi wa chumba cha darasa shule ya Sekondari Luagala
“Lengo la kutembelea miradi hii kwa wakuu wa Idara mbalimbali na vitengo ndani ya Halmashauri yetu ni kujionea kwa macho hatua iliyopo na kuifahamu miradi hii na kubaini changamoto zilizopo kwenye miradi hii badala ya kuwaachia wakuu wa idara husika,”amesema Machela
Wakuu wa Idara na vitengo walitembelea mradi wa ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa shule ya Msingi Mkula
Naye Mkurugenzi wa Mji mdogo Mahuta Rajabu Lwazi ambaye ni miongoni mwa waliotembelea miradi hiyo amekiri kuwa katika ziara hiyo ameweza kuifahamu miradi mingi ambayo inatekelezwa na Halmashauri
Ujenzi wa matundu ya vyoo Shule Msingi Mkulung`ulu
“Hii ziara imetusaidia sana kuifahamu miradi inayotekelezwa na Halmashauri yetu maana tangu niwe hapa sijawahi kutembelea miradi mingi kama hivi na imenisaidia kuijua na kutoa ushauri pale ambapo tunaona panahitaji ushauri,”amesema Lwazi
Wakuu wa Idara na Vitengo wakimsikiliza Afisa mtendaji akisoma taarifa ya mradi waujenzi wa nyumba ya mwalimu kijiji cha Namkomolela
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa