Na Kitengo cha Mawasiliano
Wajumbe wa Kamati ya Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) ngazi ya Kata wametakiwa kuzingatia mafunzo yatakayotolewa ili kutekeleza majukumu kwa ufanisi katika maeneo yao
Akizungumza Januari 16,2023 wakati akifungua mafunzo hayo Kaimu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Tandahimba Ndg.Ismaely Mbilinyi kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji amesema kuwa kamati hizo zinatakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano ili kutokomeza vitendo vya ukatili katika maeneo yao
“Mafunzo haya ni muhimu kuyazingatia ili mkatekeleze kwa ufanisi majukumu katika maeneo yenu ,”amesema Mbilinyi
Kwa upande wa wawezeshaji wa mafunzo wamewasilisha mada nne kwa washiriki kwa siku ya kwanza ikiwa ni miongoni mwamada 11 ambazo zitawasilishwa katika mafunzo hayo
Mafunzo hayo ya siku tatu yatahitimishwa Januari 18,2023 ambapo Wajumbe Kata nane ambazo ni Litehu,Ngunja,Nambahu,Mkonjowano,Chaume,Luagala,Lyenje na Mkwedu wanashiriki mafunzo hayo ikiwa ni muendelezo wa mafunzo ya Mtakuwwa yanayotolewa ngazi ya kata
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa