Waheshimiwa Madiwani
Na Kitengo cha Mawasiliano
Waheshimwa Madiwani na baadhi ya Wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba wamefanya ziara ya siku Mbili Halmshauri ya Jiji la Mbeya ili kujifunza Uanzishaji na Uendeshaji wa Shule za Msingi za lugha ya kiingereza(English Medium) zinazomilikiwa na Halmashauli,Usimamizi na Uhifadhi wa taka ngumu na usafi wa mazingira na namna ya ukusanyaji wa mapato ya ushuru wa huduma
Baadhi ya Wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba walioambatana na Waheshimiwa madiwani katika ziara
Ziara hiyo ya siku mbili imeanza Februari 21,2023 ambapo Mchumi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya aliwasilisha taarifa ya uanzishaji na ubunifu wa shule hizo na jinsi zinavyoongeza mapato ya Halmashauri ya Jiji hilo
Aidha amesema kuwa mbali na Halmashauri kupata mapato lakini pia wanatoa huduma kwa wananchi wenye kipato cha kawaida kuweza kuwasomesha watoto wao kwa gharama nafuu
Naye Mkuu wa kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu wa Jiji la Mbeya akisoma taarafa yake jinsi walivyofanikiwa amebainisha kwamba jukumu hilo limekasimishwa ngazi ya kata ambapo njia hiyo imefanikiwa kuweka mazingira katika hali ya usafi
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa