Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala amepiga marufuku kwa wafugaji kuingia katika Wilaya ya Tandahimba bila kufuata taratibu na sheria ili kuepuka migogoro isiyo ya lazima katika jamii iliyopo eneo husika
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala akieleza jambo kwa wananchi wa kijiji cha Dinyeke
Ameyasema hayo kwenye ziara yake ya kujitambulisha na kusikiliza kero za wananchi wa kijiji cha Chikongo na Dinyeke kata ya Mkoreha ambapo amesema ili wafugaji wapewe eneo lazima wafuate taratibu kama hakuna taratibu ambazo zimefuatwa katika eneo husika wanapaswa kuondolewa haraka
Wananchi wa kijiji cha Chikongo wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba(hayupo pichani)
“Mifugo tunaipenda lakini lazima utaratibu ufuatwe na wananchi waambiwe katika kijiji husika,lakini kama mfugaji hajafuata taratibu na kibali hana lazima aondoke ili kuepusha migogoro katika jamii ambayo inaweza kusababisha uvunjifu wa amani katika eneo husika hilo halikubaliki na hatua kali za kisheria tutachukua,”amesema Dc Sawala
Wataalamu wakifuatilia maswali ya wananchi kuhusu masuala mbalimbali ambayo ni kero kwa wananchi wa Dinyeke
Aidha akiwa katika vijiji hivyo amezungumzia masuala mbalimbali ikiwemo Elimu,Afya,maji,umeme,kilimo na ushirika,barabara,ulinzi na usalama na ushiriki wa wananchi katika miradi ya maendeleo pia amesistiza wananchi katika msimu huu ulioanza wahakikishe wanauza korosho zao kwenye vyama vyao vya msingi ili waweze kupata fedha zitakazoongeza maendeleo ya kijiji chao
Wananchi walitoa kero zao kuwa ni pamoja na upungufu wa walimu,mifugo,maji,umeme,barabara,zahanati ambapo majibu ya kero zao zilijibiwa na wataalam walioambatana na Mkuu wa Wilaya katika ziara yake
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa