Na.Kitengo cha Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Michael Mntenjele amewasisitiza wadau wa Maendeleo na Wananchi kujikita katika kutoa maoni yenye manufaa kuhusu Mwelekeo wa maendeleo wanayotaka kuyafikia ifikapo 2050.
"Suala hili ni la Kitaifa hivyo kila Mwananchi anatakiwa kufikiria na kutoa Maoni kwamba kwa miaka 25 ijayo ataitaka Tanzania kuwa ya namna gani katika Nyanja za kiuchumi na kijamii" Kanali.Mntenjele
Baadhi ya wadau wametoa maoni yao ikiwemo Suala la Upatikanaji wa Huduma ya Maji Vijijini ifikie 100 % ifikapo 2050 kutoka 85 % iliyokuwepo, huku wakidai Gharama za Umeme zipunguzwe ili Wananchi waweze kumudu Gharama na kuwezesha nishati ya Umeme kupatikana Katika maeneo yote Nchini ifikapo 2050.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliandaa na kuridhia kutumika kwa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 inayofikia ukomo Mnamo Juni 2026 na utekelezaji wake umewezesha Nchi kupata Mafanikio Mbalimbali ya kiuchumi na kijamii ikiwemo Nchi kuingia katika kundi la Nchi za kipato Cha Kati.
Aidha, Mnamo Desemba 9, 2023 Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan alizindua Rasmi zoezi la ushirikishaji wadau na ukusanyaji wa maoni ya Wananchi kuhusu Dira Mpya 2050 ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba imefanya Kikao Cha kukusanya Maoni hayo kutoka kwa wadau na Wananchi Leo Julai 22, 2024 katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri.
#kaziiendelee
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa