Na Kitengo cha Mawasiliano.
Wadau wa Korosho Wilaya ya Tandahimba na Newala wameweka mikakati ya kudhibiti ubora wa Korosho ili kuongeza thamani ya bei kwa wanunuzi wanaokuja kununua korosho hizo
Akifungua kikao hicho Oktoba 26,2023 Katika ukumbi wa mikutano wa Wilaya ya Newala, Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe.Alhaji Mwangi Rajabu Kundya amesema thamani ya korosho inapoongezeka wanufaika ni wakulima wa zao hilo
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala amewasistiza maafisa Ugani,Maafisa Ushirika na Viongozi wa Vyama vya Ushirika kuendelea kutoa elimu kwa Wakulima ya ukaushaji wa korosho na kuhifadhi katikaviwango vinavyotakiwa huku akiwataka watunza maghala kusimamia ubora wa korosho kwa kuzingatia vipimo vya unyevu kabla ya kuingiza ghalani.
Katika hatua nyingine viongozi hao wakiwemo wa vyama vya ushirika (AMCOS) na watunza Maghala kwa pamoja wameahidi kusimamia kwa weledi majukumu yao pamoja na kuzingatia maelekezo waliyopewa ili kuendelea kulinda ubora wa korosho hizo.
Mpaka sasa Wilaya ya Tandahimba inaongoza kwa uzalishaji wa korosho bora nchini Tanzania .
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa