Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala amesema kuwa maazimio ambayo wameyaweka katika kikao cha wadau wa elimu yakisimamiwa na kufuatiliwa yataleta matokeo yenye tija na kuongeza ufaulu
Ameyasema hayo leo Januari 25,2022 kwenye kikao maalum cha wadau wa Elimu ambacho kimeazimia kuongeza ufaulu kwa kuyasimamia yale ambayo wadau wamekubaliana katika kikao hicho sambamba na kuyafuatilia kuhakikisha malengo yanafikiwa
“Tunaondoka hapa na kamapeni yetu ya kuondoa ziro kwa kidato cha nne na kidato cha pili,lakini pia kwa darasa la nne tunaondoa alama za D&E kwenye matokeo yao kwa kusimamia maazimio yetu ambayo tumejiwekea,hatujachelewa muda wa kufanya vizuri tunao,”amesema Dc Sawala
Aidha amesema kuwa ili mafanikio yawe mazuri zaidi ushirikiano kati ya mwalimu,mzazi na mwanafunzi uimarishwe ili kuweza kufuatilia maendeleo ya mwananfunzi kwa karibu na hivyo kuwasistiza wazazi kutoa ushirikiano wa dhati kwa walimu
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba ndugu Mussa Gama amesema kwakuwa maazimio yamefanyika kwa pamoja jukumu kubwa ni wakuu wa shule Sekondari na Msingi,waratibu kata,watendaji kata na maafisa tarafa kuhakikisha wanatekeleza wajibu wao ili kufikia malengo
“Naamini katika vitendo zaidi kila mmoja atimize wajibu wake ili tuweze kufikia maazimio yetu tuliyokubaliana hapa wote kwa pamoja suala la lishe tutalisimamia ili wanafunzi waweze kusoma na kuelewa wanahitaji kupata chakula hili tutalisimamia,”amesema Mkurugenzi
Nao washiriki wa kikao hicho wamempongeza Dc kwa kuahidi kushirikiana nao ili kuinua Elimu Wilaya ya Tandahimba na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano ili kuyafikia maazimio
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa