Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Wadau mbalimbali wametoa vifaa tiba kwa ajili ya mampambano dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa Covid -19 kuunga mkono jitihada za Mkuu wa Wilaya ya Tandhaimba Sebastian Waryuba ili wananchi waendelee kuwa salama
Dc Waryuba akiwa na Mkurugenzi Mtendaji Said Msomoka, Katibu Tawala Benaya Kapinga na maafisa wengine wakati wa makabidhiano ya vifaa nje ya ofisi yake
Wadau ambao wameweza kutoa michango mbalimbali ya vifaa tiba kwa ajili ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa Covid -19 ni pamoja na Baraza la madiwani,watumishi,wadau wa elimu ,Chama cha Walimu,Benki ya NMB,Benki ya CRDB na baadhi ya Wafanyabiashara ndani ya Wilaya
Baraza la madiwani wamechangia kila mmoja fedha kwa ajili ya mapambano ya Corona
Akizungumza baada ya Kukabidhi vifaa tiba Afisa Elimu Msingi Hadija Mwinuka amesema kuwa jitihada hizo zinachukuliwa ili kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Covid -19 ndani ya Wilaya wananchi waweze kuwa salama na kuendelea na shughuli za maendeleo
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji ahmada Suleiman akipokea vifaa kutoka kwa Afisa Elimu Msingi Hadija Mwinuka
“Vifaa hivi vimetolewa na Wadau mbalimbali wa elimu ,watumishi wa elimu pamoja na Chama cha Walimu (C.W.T) ikiwa ni jitihada za kuunga mkono agizo la Mkuu wa Wilaya la kila mtu aweze kuchangia katika mapambano haya ili Wilaya yetu iendelee kuwa salama kwa kujikinga na maambukizi,”amesema Mwinuka
Baadhi ya Watumishi wa Halmashauri ya Tandahimba ambao nao wamechangia fedha katika mapambano ya Covid -19
Naye Meneja wa NMB tawi la Tandahimba Julietha Ndazi amesema watumishi wameweza kutoa ndoo za kunawia mikono ili kuunga mkono kauli ya Mkuu wa Wilaya katika mapambano dhidi ya maambukizi ya Covid -19
Meneja wa Nmb Tawi la Tandahimba Julietha Ndazi akikabidhi vifaa hivyo
Aidha Meneja wa CRDB tawi la Tandahimba Emmanuel Hitla amesema mapambano dhidi ya maambukizi ya Covid -19 ni ya kila mmoja hivyo ili shughuli za maendeleo ziendelee inahitaji wananchi wawe salama kwa kujikinga na virusi vya Corona
Meneja wa Crdb Tawi la Tandahimba Emmanuel Hitla akikabidhi vifaa kwa Kaimu Mkurugenzi Ahmada Suleiman
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa