Ikiwa ni siku ya kwanza ya mafunzo kwa Waandishi Wasaidizi na Waendesha Vifaa vya bayometriki Jimbo la Tandahimba wametakiwa kushirikiana sambamba na kuvitumia vifaa hivyo kwa usahihi huku wakitakiwa kufanya kazi hiyo kwa uadilifu.
Akifungua mafunzo hayo ya siku mbili Januari 25,2025 yanayofanyika kwenye Shule ya Sekondari ya Tandahimba Afisa Mwandikishaji Jimbo la Tandahimba Ndg.Aloyce Massau amesema kuwa vifaa watakavyokabidhiwa vitunzwe ili kufanikisha zoezi la Uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura.
" Mafunzo haya yakawasidie kufanya kazi kwa uadilifu na ushirikiano kwenye maeneo yenu .mmeaminiwa tunaimani mtafanya kwa weledi mkubwa,pia mkavitunze vifaa hivi ambavyo vitawasidia katika utekelezaji wa zoezi hili," amesema Massau.
Uboreshaji wa daftali la kudumu la wapiga kura Jimbo la Tandahimba litaanza rasmi Januari 28,2025 hadi Februari 3,2025 ambapo kauli mbiu "Kujiandikisha kuwa Mpiga kura ni Msingi wa Uchaguzi Bor
a"
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa