Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba ndugu Mussa Gama amewaomba wakulima kuchangamkia mbegu za ufuta na alizeti zinazotolewa bure na Halmashauri kupitia Idara ya kilimo
Mkurugenzi Mtendaji ndugu Mussa Gama akitoa majibu kwa madiwani
Amesema kuwa Halmashauri ya Tandahimba inatarajia kuwekeza viwanda vidogo vitatu vya kukamua mafuta ya alizeti katika Tarafa tatu ya Litehu,Namikupa na Mahuta ambapo zinatasaidia mkulima kuuza zao hilo kwa urahisi
Wakuu wa Idara na vitengo walioshiriki kwenye kikao cha baraza la madiwani
Ameyasema hayo kwenye kikao cha kawaida cha baraza la madiwani baada ya kusoma taarifa yake na Mhe.Hamza Balakali Diwani wa kata ya kwanyama kuhoji uhakika wa soko kwa wakulima ambao zao la alizeti katika Wilaya yao ni jipya kibiashara
Waheshimiwa madiwani wakiwa kwenye kikao katika ukumbi wa mikutano
“Halmashauri tunaendelea kusambaza mbegu za alizeti kilo 300 na ufuta kilo 3000,niwaombe madiwani wahimizeni wananchi kulima na mazao mbadala ya kibiashara kama alizeti na ufuta,Halmashauri tunatarajia kuwekeza viwanda vidogo vitatu vya kukamua mafuta ya alizeti kwaiyo soko litakuwepo hapa hapa Tandahimba,”amesema Mkurugenzi
Aidha akitoa muelekeo wa bei za viuatilifu katika maandalizi ya msimu ujao amesema utaratibu ambao umeandaliwa ni mkulima kuchangia asilimia 50 ya bei ya sokoni na serikali asilimia 50 ambapo utaratibu utaratibiwa na chama kikuu kwa kushirikiana na vyama vya msingi
Naye Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe. Kanali Patrick Sawala amewasistiza madiwani kuhakikisha katika maeneo yao wananfunzi waliochaguliwa kidato cha kwanza wanakwenda shule lakini pia wananfunzi wanaotakiwa kuanza darasa la kwanza na awali wanapelekwa shule kwa wakati
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala akisistiza jambo kwa madiwani
“Sioni sababu ya wanafunzi hadi leo kutoripoti shuleni,nawaomba madiwani mkalisimamie hili katika maeneo yenu,mwanafunzi ambaye hataripoti shule hatua kali tutamchukulia mzazi wake,katika hili tutakua wakali kwasababu Mhe.Rais amejenga miundombinu mizuri,hata kama mwanafunzi hana sare za shule aripoti shule mengine yatafuata,”amesema Dc Sawala
Waheshimiwa madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba
Katika kikao hicho cha siku mbili madiwani waliweza kuwasilisha taarifa zao za maendeleo ya kwenye kata zao sambamba na kumshukuru Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa ujenzi wa vyumba 88 vya madarasa ambavyo vimewezesha wanafunzi wote waliochagulia kuingia madarasani kwa wakati mmoja
Madiwani wakiwasilisha taarifa za kamati
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa