Na Kitengo cha Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala akiwa pamoja na KU,Mkurugenzi Mtendaji Halmasahauri ya Wilaya ya Tandahimba Ndg.Mussa Gama na na Wakuu wa Idara na Vitengo wameshiriki kujaza kifusi mradi wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa shule ya sekondari Lukokoda
Mradi huo umeibuliwa na wananchi wa Kata ya Lukokoda ambapo shughuli ya ujazaji wa kifusi umefanyika Machi 7,2023 kwa kushirikiana na wananchi ambao wamejitokeza kwa wingi ikiwa ni kuamsha ari kuelekea siku ya wanawake Machi 8,2023
Akizungumza mara baada ya kukamilisha shughuli ya kujaza Kifusi Dc Sawala amewapongeza wananchi kwa kuibua mradi huo ambao utawanufaisha wanafunzi wa kata hiyo lakini kushiriki katika miradi ya maendeleo
“Nawapongeza kwa kuibua mradi huu lakini pia kwa ushiriki wenu katika miradi ya maendeleo,tumekuja kushiriki na wananchi wa kata ya lukokoda ili kuunga juhudi mnazozifanya,lakini pia tunaelekea siku ya wanawake ikaamshe ari kwenu kushiriki katika maadhimisho haya,”amesema Dc Sawala
Aidha amewasistiza wananchi kupinga ukatili wa jinsia ambao unafanyika katika jamii kwa kutoa taarifa katika vyombo husika ili viweze kuchukua hatua stahiki kwa muhusika ili kutokomeza vitendo hivyo
Naye Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Ndg.Gama kuunga juhudi za wananchi katika mradi huo Halmasahauri imekabidhi saruji mifuko 20 ili iweze kusaidia katika mradi huo
“Halmashauri kwa kutambua mchango wenu wa kuibua mradi huu tunakabidhi mifuko hii ili ikaongeze nguvu katika mradi huu uweze kukamilike kwa wakati wanafunzi wetu waweze kutumia madarasa haya,”amesema Mkurugenzi
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa