Na Kitengo cha Mawasiliano
Timu ya Viongozi wa Mkoa na Halmashauri za Mkoa wa Mtwara wamefika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi kwa ajili ya kujifunza Biashara ya Hewa Ukaa.
Akizungumza wakati akiwapokea Mkuu wa Mkoa huo Mhe.Mwanamvua Mrindoko amesema Biashara ya Hewa Ukaa inalipa na kuongeza kuwa mbali na fedha zinazopatikana katika Biashara hiyo, Misitu hiyo inasaidia kutunza Mazingira pamoja na kuzalisha ajira kwa Wananchi.
Akizitaja baadhi ya faida hizo RC Mrindoko amesema ."Hamkufanya kosa kuja Katavi, kwenye Hewa Ukaa tulianza 2018, tuna vijiji 8, vimeingiza Bilioni 8.2 na katika fedha hizo tumetekeleza miradi zaidi ya 30 na Mwezi Januari tunatarajia kupokea Zaidi ya Bilioni 14"
Akitoa Salamu Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara , Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mwanahamisi Mkunda amesema Mkoa wa Mtwara unatarajia kunufaika baada ya kujifunza kutokana na Misitu iliyopo katika Mkoa huo inayotokana na Miti ya Mikorosho na kuongeza kuwa Ziara hiyo ya Siku tatu italeta tija katika Mkoa huo
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa