Na Kitengo cha Mawasiliano
Viongozi na Wananchi wa Mkoa wa Mtwara wameshuhudia utiaji saini wa Mkataba wa Ujenzi wa Barabara ya Mnivata hadi Masasi Km160 itakayojengwa kwa kiwango cha lami ambapo kiasi cha Shilingi Bilioni 234.5 zitatumika kutekeleza mradi huo ambao utakamilika Mwaka 2025
Hafla ya utiaji saini wa Mkataba huo umefanyika Juni 21,2023 katika uwanja wa Sabasaba Halmashauri ya Mji Newala ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof.Makame Mbarawa
Ujenzi wa barabara hiyo utatekelezwa na Makampuni mawili ambapo Km 100 zitajengwa na Kampuni ya China Wi Yi ambayo itaanzia Mnivata hadi Mitesa kwa thamani ya shilingi Bilioni 141.9 na Km 60 zitajengwa na Kampuni ya China Communication Construction ambayo itaanzia Mitesa hadi Masasi Mjini kwa thamani ya shilingi Bilioni 92.5
Aidha Ujenzi wa Barabara ya Mnivata,Nanyamba, Tandahimba, Newala na Masasi kwa kiwango cha lami itafungua fursa ya kiuchumi kwa wananchi wa Mtwara ambao wameipongeza Serikali kwa kutatua kero yao ya barabara hiyo
Kwa upande wao wabunge wa Mkoa wa Mtwara ambao walihudhuria hafla hiyo wameipongeza Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuwakumbuka watu wa Mtwara
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa