Na.Kitengo cha Mawasiliano.
Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini ( RUWASA) Wilaya ya Tandahimba Mhandisi. Antidius Muchunguzi amesema Serikali ilitoa Fedha kiasi Cha Tsh.Bilioni 6.5 kwa ajili ya Ujenzi wa Miundombinu ya Maji katika Kata Nne za Wilaya hiyo Mradi ambao utakamilika na Kuanza kutumika Mwezi Novemba, 2023.
Mhandisi Muchunguzi ameyasema hayo leo Oktoba 3,2023 wakati akisoma taarifa ya Maendeleo ya Ujenzi wa Mradi wa Maji Mkwiti na kuongeza kuwa Mradi huo ukikamilika unatarajia kuwahudumia wakazi wapatao 26,164 wa kata Nne za Mangombya, Ngunja, Litehu na Luagala .
"Jumla ya Vioski 45 vimejengwa katika vijiji 17 kwa ajili ya kuchotea maji na kuunganisha huduma ya maji katika taasisisi, Zahanati na Vituo vya Afya katika vijiji vyote 17 ambapo ongezeko hili litafanya watu wanaopata huduma ya maji Tandahimba kuongezeka kutoka asilimia 50 ya sasa hadi kufikia asilimia 60.2," amesema Mhandisi Muchunguzi
Aidha, Wajumbe wa Kamati ya Siasa Wilaya wameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe Rais Dokta Samia Suluhu Hassan na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa (CCM) kwa kuufanya Mradi wa Maji Mkwiti kuwa miongoni mwa miradi inayoenda kuondoa kero ya maji kwa wananchi.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa