Na Kitengo cha Mawasiliano
Kuelekea uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Mkoani Mtwara Aprili 1,2023 Vijana wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba wakiongozwa na Katibu Tawala Wilaya ya Tandahimba Ndg. Juvenile Mwambi wameshiriki kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira katika hospitali ya Wilaya ya Tandahimba
Zoezi la Upandaji miti limefanyika Machi 21,2023 katika shule ya msingi Nandonde na nje ya uwanja wa mpira wa Majaliwa katika Kata ya Tandahimba
Aidha Katibu Tawala amewapongeza vijana kwa kushiriki lakini pia ametoa wito kwa vijana wa Tandahimba kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Mkoani Mtwara na kuupokea Mwenge wa Uhuru Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Aprili 5,2023 katika kata ya Miuta
Kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 “Tunza Mazingira Okoa Vyanzo vya maji kwa Ustawi wa viumbe hai na Uchumi wa Taifa”
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa