Na Kitengo Cha Mawasiliano
Upepo Mkali umeezua paa la vyumba viwili vya madarasa na ofisi moja ya walimu na kusababisha wanafunzi kumi na tatu (13) waliokuwepo ndani ya darasa kupata majeraha katika shule ya Msingi Amani iliyopo Kata ya Tandahimba Halmashauri ya Wilaya yaTandahimba
Tukio hilo limetokea leo Septemba 14,2022 saa 8.15 mchana ambapo upepo baada ya kuezua sehemu ya paa hilo liliangukia ndani ya darasa la tatu ambapo walikuwemo wanafunzi wanaendelea na masomo na kuwajeruhi baadhi ya wanafunzi
Wanafunzi hao 13 wote walipelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Tandahimba kwa ajili ya matibabu ambapo Dk.Fatuma Juma ambaye alikuwa zamu amesema kuwa amewapokea wanafunzi 13.,wanafunzi 12 walipata majeraha madogo madogo na wengine ni mshtuko wametibiwa na wameruhusiwa kurudi nyumbani na mwanafunzi mmoja amelazwa kwa matibabu zaidi
“Nimewapokea wanafunzi 13 ambapo wasichana idadi yao ninane (8) na wavulana watano(5) hawa kumina mbili baadhi walikuwa majeraha madogo madogo tumewatibu lakini wengine ni mshtuko tunashukuru wote wanaendelea vizuri tumewaruhusu warudi nyumbani,mmoja amelazwa kwa ajili matibabu zaidi,”amesema Dk.Fatuma
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala akiwa pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Ndg.Robert Mwanawima na Kamati ya Usalama Wilaya walifika shuleni hapo kuangalia hali halisi baadaye walifika hospitali kutoa pole kwa wanafunzi hao
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa