Na Kitengo cha Mawasiliano
Katibu Tawala Wilaya ya Tandahimba Ndg.Juvenile Mwambi na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmasahauri ya Wilaya ya Tandahimba Ndg.Robert Mwanawima wamewahakikishia wananchi walioathirika na mvua katika Kata ya Mndumbwe na Milongodi kuwa Serikali ipo pamoja nao na hatua za awali zimechukuliwa
Akizungumza Novemba 16,2022 kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Ndg.Juvenile Mwambi akiwa na wajumbe wa Kamati ya Maafa Wilaya wametoa pole kwa wananchi wa Kijiji cha Mambamba,Majengo na Namkomolela walioathirika na maafa hayo
Mvua iliyoambatana na Upepo Mkali iliyotokea Novemba 15,2022 imeharibu Jumla nyumba 43 za wananchi wa Kijiji cha Mambamba na Majengo Kata ya Mndumbwe lakini pia imeaharibu Miundombinu ya Chumba kimoja cha Darasa Shule ya Msingi Namkomolela iliyopo Kata ya Milongodi
Hata hivyo baadhi ya waathirika waliotembelewa katika maeneo yao wameipongeza Serikali kwa kujali wananchi wake kwa kufika na kuona hali halisi ikiyojitokeza baada ya maafa hayo
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa