Na Kitengo cha Mawasiliano
Wawezeshaji wa masuala ya kutokomeza ukatili wa kijinsia wametakiwa kwenda kuelimisha na kuwawezesha wengine katika jamii kufahamu athari za ukatili wa kijinsia na hatua za kuchukua kukomesha tatizo hilo.
Hayo yamesemwa leo Desemba 13,2024 na Afisa Usimamizi Fedha Mkoa wa Mtwara CPA.Norbert Shee kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara kwenye mafunzo ya wawezeshaji wa masuala ya kutokomeza Ukatili wa kijinsia yaliyofanyika Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba.
" Tunawashukuru wadau wetu Shirika la Umoja wa Mataifa la UN Women kwa kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali,ambapo mafunzo haya yatawezesha washiriki kupata uelewa na maarifa sahihi juu ya afua za ukatili wa kijinsia na mbinu za kukabiliana nao, " amesema Shee
Kwa.upande wao wawezeshaji wa mafunzo hayo wamewasilisha mada mbalimbali ambapo pia wamesistiza ushirikiano katika kupambana na ukatili wa kijinsia katika jamii kwakuwa madhara yake ni pamoja na kuleta umaskini katika Kaya na Jamii kwa ujumla.
Mafunzo hayo yamewezeshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia .masuala ya Usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji wa wanawake ( UN WOMEN) kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa