Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Michael Mtenjele amewasisitiza Wananchi Wilayani humo kushiriki katika ulinzi Shirikishi.
DC Mtenjele ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani Robo ya tatu(Januari -Machi 2024) uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri.
"Rudisheni ulinzi shirikishi kama ilivyokuwa mwanzo kwa kuzingatia Sheria na taratibu , suala la ulinzi na salama ni la kila Mtanzania kwa kuwa palipo na amani shughuli za Maendeleo zitafanyika" Kanali Mtenjele
Aidha, DC Mtenjele amewaonya watu watakaokwamisha zoezi la ulinzi shirikishi kwa maslahi yao binafsi akiwataka kuacha mara moja.
#kaziiendelee
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa