Na Kitengo cha Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala amevitaka vyombo vyote vinavyosimamia haki ndani ya Wilaya ya Tandahimba kuwajibika kila mmoja kwa nafasi yake ili haki itendele kupinga vitendo vya kikatili visiendelee katika jamii
Amesema hayo Disemba 6,2022 katika Kongamano la maadhimisho ya siku 16 za kupinga Ukatili Kiwilaya ambalo limefanyiuka katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashgauri na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali
“Vitendo vya ukatili katika Wilaya yetu vipo,natoa rai usikae kimya ukifanyiwa vitendo vya ukatili vyomba vipo vya kushughulikia haki,vyombo vya kusimamia haki hakikisheni kila mtu kwa nafasi yake anatekeleza wajibu wake ili haki itendeke ,”amesema Dc Sawala
Aidha ameeleza kuwa ndani ya familia kila mmoja atambue wajibu na haki yake,uhuru upo katika kufanya kazi kwa bidii kwakuwa wanawake wanaweza katika Nyanja mbalimbali
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Door of Hope Tanzania Ndg.Clemence Mwombeki amesema rushwa ya ngoni moja ya ukatili unaoondoa utu hivyo jukumu la wadau ni kushirikiana na Serikali katika kuchukua hatua za kupinga ukatili
Kongamano lilihudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo wawakilishi kutoka Ubalozi wa Canada ,maadhimisho ya siku 16 za kupinga Ukatili wa kijinsia yalianza Novemba 25,2022 ambapo Kiwilaya imeadhimishwa kwa kutoa elimu katika makundi mbalimbali na kuhitimisha kwa kongamano lililowashirikisha wadau
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa