Na Kitengo cha Mawasiliano
Mwenyekiti wa Halmasahauri ya Wilaya ya Tandahimba Mhe.Baisa Baisa amesema kuwa ili Bajeti iweze kutekeleza mipango iliyopangwa ni jukumu la madiwani na wataalamu wa Halmasahauri kusimamia ukusanyaji wa mapato ili mipango itekelezeke
Amesema hayo wakati akifunga kikao Maalum cha Baraza la Madiwani cha Mapendekezo ya Mpango na bajeti ya Halmasahauri kwa mwaka wa fedha 2023/2024 kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri Januari 6,2023
“Tusimamie na kuimarisha ukusanyaji wa mapato yetu ya ndani ili yale ambayo tumepanga yatekelezeke,tusitegemee vyanzo vichache kama vile korosho, tunavyo vyanzo vingi tukisimamia mapato yetu yataongezeka na yote ambayo yapo kwenye mpango yatafanyika ,”amesema Mwenyekiti
Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba imejiwekea lengo la kukusanya na kutumia shilingi 5,558,727,900 kwa mwaka wa fedha 2023/2024 kutoka katika vyanzo vyake vya ndani vya mapato
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa