Na Kitengo cha Mawasiliano.
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala amesema Serikali ya Awamu ya Sita imefanya mageuzi makubwa katika kutoa huduma za Msingi kwa Jamii ikiwemo maji ambapo Wilaya hiyo imenufaika na Miradi ya maji inayotekelezwa kwa Wananchi ikilinganishwa na miaka ya Nyuma.
DC Sawala ameyasema hayo Leo Desemba 21, wakati akifungua Mkutano wa Nusu Mwaka wa Wadau wa Maji uliofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri hiyo.
"Hali ya upatikanaji wa Maji katika Wilaya yetu kwa sasa hauwezi kulinganisha na Miaka Miwili iliyopita ambapo ilikuwa Chini ya 20% lakini kwa sasa inakwenda mpaka 51% ni jitihada kubwa zimefanywa na zinaendelea kufanywa na Serikali yetu ya Awamu ya Sita" DC Sawala
Sambamba na hilo DC Sawala amewapongeza Viongozi wa RUWASA na MAKONDE kwa kuendelea kusimamia vyema upatikanaji wa Maji kwa Wananchi pamoja na Miradi Mikubwa ya Maji inayoendelea kujengwa Tandahimba huku akiwaasa Jumuiya za Maji kuhakikisha zinasimamia vyema ukusanyaji wa mapato ili Miradi hiyo ya Maji iendelee kujiendesha.
Kwa Upande wake Meneja wa RUWASA Wilaya ya Tandahimba Mhandisi Antidius Muchunguzi amesema mpaka sasa Wananchi 152,658 kati ya wananchi 299,073 wanapata huduma ya maji sawa na 51% na kuongeza kuwa ifikapo Mwaka 2025 Hali ya upatikanaji wa Maji itafikia 90%.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa