Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba DCI. Mariam Mwanzalima amewasistiza Waandishi Wasaidizi na Waendesha Vifaa vya Bayometriki kutoa huduma bora kwa wananchi kwenye zoezil a Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga
Amesema hayo Januari 26,2024 alipowatembelea washiriki kwenye mafunzo yao Shule ya Sekondari Tandahimba ikiwa ni siku ya Pili ya mafunzo hayo ambapo amewaeleza.kuwa wameaminiwa wahakikishe wanafanya kazi hiyo kwa uadilifu na kutoa huduma bora kwa wananchi.
" Mkatoe huduma bora kwa wananchi wakati wote wa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura huku mkizingatia makundi maalumu na matumizi ya lugha nzuri pamoja na kuwepo wakati wote kwenye vituo vya kuandikisha wapiga kura," amesema Ded Mwanzalima
Mafunzo hayo yamehitimisha lJanuari 26,2025 na Afisa Mwandikishaji Msaidizi Jimbo la Tandahimba Ndg.Skeba Bukuku ambapo amewahimiza kuzingatia muda sahihi wa kufungua na kufunga vituo vya kuandikisha.
Washiriki 728 kutoka Kata 32 wa Jimbo la Tandahimba kawenye mafunzo hayo ya siku mbili wamejifunza ujazaji wa Fomu mbalimbali pia wamejifunza kwa nadharia na vitendo namna ya kuandikisha wapiga kura kwa kutumia mfumo wa kuandikisha wapiga kura (VRS )ikiwa pamoja na kuchukua taarifa binafsi za mwombaji na taarifa za kibayometriki za mwombaji na kisha kuchapisha kadi ya mpiga kura.
#Tandahimba tumejipanga kazi zinaendelea
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa