Na Kitengo cha Mawasiliano
Timu ya Wilaya ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba imetembelea kukagua shule hadi shuleza sekondari katika kata ili kuang kuona hali halisi ya uripoti wa wanafunzi hususani wa kidato cha kwanza
Ziara hiyo imekamilika Januari 19,2023 ambapo Dc Sawala ameendele kusistiza wanafunzi wa kidato cha kwanza ,walisajiliwa awali na darasa la kwanza waripoti shule ambapo ametoa siku saba hadi kufikia Januari 23,2023
Aidha amewasistiza Wakuu wa Shule kuwapokea wanafunzi hao hata wasipokuwa na sare za shule ili waendelee na masomo ”Nawapongeza walimu sijapata malalamiko yoyote ya mzazi kuwa mnawakataa wanafunzi wasiokuwa na sare,wapokeeni wanafunzi wote hata wasiokuwa na sare ili wapate haki yao ya msingi ambayo ni Elimu”amesema Dc Sawala
Katika ziara hiyo Timu zote tatu zimezungumza na uongozi wa Kata husika na walimu wa shule husika ili kuhakikisha wanafunzi wanaripoti shule kwa asilimia 100
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa