Na Kitengo cha Mawasiliano
Timu ya ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba ikiongozwa na Mkuu wa Idara ya Elimu ya awali na Msingi ndg.Samweli Mshana wamefanya ziara ya kufuatilia na kuona maendeleo ya ujenzi wa nyumba za walimu,umaliziaji wa vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo
Ziara hiyo yenye lengo la kuangalia maendeleo ya miradi hiyo imefanyika Februari 18,2023 kuona changamoto zilizopo na kuweza kuitatua ili iweze kukamilika kwa wakati uliopangwa
Miradi ambayo imetembelewa na timu hiyo ni Ujenzi wa nyumba ya mwalimu shule ya msingi Mkwiti,,ujenzi wa nyumba ya mwalimu shule ya msingi Amani iliyopo Chaume,ujenzi wa mradi wa nyumba ya mwalimu shule ya msingi Mkwedu,umaliziaji wa chumba kimoja shule ya msingi Malamba,umaliziaji wa chumba kimoja shule ya msingi Nanhyanga A,Umaliziaji wa mradi wa vyumba viwili vya madarasa shule ya msingi Nanhyanga B
Miradi mingine iliyopitiwa na timu hiyo ni umaliziaji wa vyumba viwili vya madarasa shule ya msingi Namikupa II ambapo walisistiza kuzingatia mipango kazi yao ili miradi hiyo ikamilike
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa