Pichani: Wanufaika wa Mpango wa kunusuru kaya masikini kijiji cha Matogoro kata ya Tandahimba wakisubiri malipo huku wengine wakiwa wamelala.
Na Kitengo cha Habari na Masiliano
“Zaidi ya shilingi milioni mia mbili na kumi na moja (Tsh. 211,948,000/=) zategemewa kulipwa kwa walengwa elfu sita mia nane sabini na tisa wa kaya maskini wilayani Tandahimba” Ndugu Ismail Mbilinyi, Mratibu wa TASAF wilaya ya Tandahimba alisema.
Ndugu Ismail Mbilinyi, alisema Walengwa hao wa kaya masikini ni kutoka vijiji themanini na nane (88) wilayani Tandahimba walianza kupokea fedha za ruzuku kwa kaya masikini tangu jana tarehe 05/02/2020 na zoezi hilo linategemewa kukamilika ndani ya siku nne.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti tofauti, baadhi ya wanufaika na mpango wa kunusuru kaya masikini unaotekelezwa na TASAF wilayani Tandahimba, wameishukuru serikali kwa kuwaletea fedha kwa wakati, “Tunaishukuru serikali ya Awamu ya Tano kwa kutujali na kutuletea fedha kwa wakati”, baadhi ya walengwa walisikika kwa furaha.
Licha ya furaha walizonazo walengwa hao, wanasikitishwa na taarifa zilizosambaa kuwa kuwa mpango wa kunusuru kaya masikini unaotekelezwa na TASAF unaelekea mwisho hali itakayopelekea ugumu wa maisha, hivyo kama ni taarifa hiyo ni sahihi wameiomba serikali kuendelea na mpango huo.
Akizungumza na Wanufaika wa Mpango wa kunusuru kaya masikini katika kata ya Tandahimba kijiji cha Matogoro, Nyamwaliki Musilikale,ambaye ni Msimamizi katika kata hiyo,amewataka wanufaika kuendeleza vikundi vyao ili kuhakikisha havifi kwani vinawasaidia katika kuleta maendeleo yao.
Bi Musilikale (Msimamizi) akiongea na walengwa juu ya utunzaji na matumizi sahihi ya fedha hizo kwa maendeleo yao
Lakini pia,Musilikale amewataka walengwa hao kuwa na vitambulisho vya Taifa ili kuepuka uwezekano wa kuwasajili raia ambao sio watanzania.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa