Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba wametakiwa kutoa ushirikiano kwa wawezeshaji ili waweze kupata taarifa sahihi ambazo zitawasaidia kwenye zoezi la mpango wa kunusuru kaya maskini wa TASAF awamu ya pili kipindi cha tatu ambapo vijiji 69 vitafikiwa katika mpango huo
Akizungumza kwenye mkutano wa kijiji cha Malopokelo Afisa Ufuatiliaji wa TASAF makao makuu Bi Judith Woiso amesema kuwa lengo la serikali ni kuwafikia wananchi wa Kitanzania ambao wanaishi katika hali duni hivyo vikao vinasaidia kuleta uwazi kwa wananchi kuwadhibitisha kwenye ngazi ya kijiji
Afisa ufuatiliaji TASAF makao makuu bi Judith Woiso(aliyesimama) akizungumza na wananchi wa kijiji cha Malopokelo
“Wananchi mnatakiwa muhudhurie kwa wingi vikao kama hivi vinasaidia kuwatambua ambao watachukuliwa taarifa zao ili mjiridhishe kwa uwazi kuwa wanastahili kuingia kwenye mpango,pia mpango huu unakuja na miradi mbalimbali ambayo itawanufaisha wananchi wote wa kijiji husika si walengwa peke yao,”amesema bi Woiso
Wananchi wa kijiji cha Malopokelo wakiwa kwenye mkutano wa kijiji na wawezeshaji wa TASAF
Wananchi wa vijiji ambavyo vimefikiwa na mpango huu wa kipindi cha pili wameishukuru serikali kwa mpango huo ambao wanatarajia utawanufaisha na kuwaondoa katika umaskini
“Tunaishukuru serikali kwa mpango wa TASAF katika vijiji vyetu ambavyo havikufikiwa tunaamini kwa wale ambao wamekidhi vigezo mpango huu utakwenda kuwasaidia na kuwawezesha kuishi maisha ya mtanzania wa kawaida angalau yakupata mlo wa siku,”amesema Kassim Mussa Mkazi wa Malopokelo
Mkazi wa Kijiji cha Malopokelo ndugu Kassim Mussa akitoa pongezi kwa serikali kwa kuleta mpango wa TASAF kijijini hapo
Mpango wa kunusuru kaya maskini kipindi cha pili awamu ya tatu Katika Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba ulizinduliwa na Mkuu waWilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba ambapo vijiji 69 sawa na asilimia 44 vitafikiwa ,awali mpango huu ulifikia vijiji 88 sawa na asilimia 56
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe. Sebastian Waryuba (kati) akiwa pamoja na wawezeshaji ngazi ya Wilaya (waliosimama),aliyekaa wa kwanza kushoto Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.Baisa Baisa,Kaimu Mkurugenzi wa ukaguzi TASAF Makao makuu ndg Shedrack Mziray ,Katibu Tawala Juvenile Mwambi na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri a Tandahimba Hadija Mwinuka
Wawezesha ngazi ya Wilaya baada ya kumaliza mafunzo wameanza kufanya utambuzi katika maeneo husika ngazi za vijiji,zoezi linaloendelea ni uchukuaji wa taarifa za kaya ambapo hadi kufikia Mei 6, mwaka huu zoezi hilo litakuwa limekamilika kwa vijiji 69 vilivyobaki ndani ya Halmashauri
Mwezeshaji wa TASAF Makao Makuu ndg Joseph Elieza akitoa mafunzo kwa wawezeshaji ngazi ya Wilaya
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa