Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala Januari 23, 2024 amepokea na Kukabidhi Mifuko 600 Kituo Cha Afya Mnyawa, Mifuko 100 Zahanati ya Mchichira pamoja na Mabati 100 Shule ya Msingi Mundamkulu iliyotolewa na Chama Kikuu Cha Ushirika Tandahimba na Newala(TANECU) ili kuunga mkono juhudi za Serikali kuwaletea Wananchi Maendeleo.
Akizungumza na Wananchi wa Kata ya Mchichira na Mnyawa kwa nyakati tofauti DC Sawala amewapongeza TANECU kwa moyo wa uzalendo na kuunga Mkono Serikali katika kuboresha huduma za Afya na Elimu Wilayani humo na kuwaasa wasimamizi wa Miradi kufanya kazi iliyokusudiwa.
"Kamati za Ujenzi simamieni, sitapenda kuona simenti inatumika nje ya kile kilichokusudiwa" DC Sawala
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa TANECU Karim Chipola amesema waliona ni vyema kile walichokipata kwenye msimu wa Korosho warudishe shukrani kwa Wananchi na kuahidi kuwa wataendelea kutoa zaidi Wananchi wapate huduma.
Aidha, Diwani wa Kata ya Mchichira Mhe.Jamari Mtonya ameishukuru TANECU kwa kuunga juhudi za Serikali kuboresha huduma na kuahidi kushirikiana nao katika kuleta Maendeleo kwa Wananchi.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa