Na Kitengo cha Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala amekabidhi mifuko ya saruji 750 yenye thamani ya zaidi ya shilingi Mil.11 na fedha taslimu Shilingi Milioni tano (5,000,000) ambayo imetolewa na Chama Kikuu cha Ushirika TANECU kwa baadhi ya Shule za Msingi na Sekondari Halmashauri ya Tandahimba
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi vifaa na fedha hizo katika ukumbi waMikutano wa Halmashauri ya Tandahimba Januari 20,2023 Dc Sawala amepongeza hatua hiyo ambayo inaleta maendeleo katika idara ya Elimu
Pichani Walimu Wakuu na Maafisa Elimu Kata ambao shule zao zimekabidhiwa saruji na fedha za vifaa
“Nawapongeza Tanecu kwa hatua hii ambayo mmefanya,ni wito wangu kwa walimu wa shule ambazo zinapokea vifaa na fedha hizi kuwa zitatumika kama zilivyokusudiwa,”amesema Dc Sawala
Kwaupande wa Mwenyekiti wa Tanecu Ndg.Karimu Chipola amesema kuwa bvifaa hivyo ni kurudisha kwa jamii kile ambacho wamekipata ambao ndiyo wadau wa Ushirika sambamba na kuunga mkono Jitihada za Mhe.Rais wa Awamu ya sita katika shughuli za Maendeleo
“Tumetoa vifaa hivi na fedha kwa shule 16 ambapo wengine wamepayta mifuko ya saruji na wengine wamepata fedha kwa ajili ya kununulia vifaa kama mashine ya kopi na kompyuta kama walivyoomba,lakini pia huu ni mwanzo tutaendelea kurudisha kile tunachokipata kwa jamii,”amesema Chipola
Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Bi.Jane Mallongo ametoa shukrani kwa Tanecu na amewahakikishia kuwa vifaa na fedha hizo zitakwenda kutumika kama ilivyokusudiwa katika idara ya elimu
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Bi.Jane Mallongo akisema jambo katika ghafla hiyo
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa