Na Kitengo cha Mawasiliano
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Dkt.Adorat Mpollo amezindua Maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji Duniani ambayo hufanyika kuanzia tarehe 1 hadi 7 Agosti kila mwaka.
Awali akizungumza wakati wa Uzinduzi huo Dkt.Mpollo amesema unyonyeshi ni muhimu katika ukuaji wa Mwanadamu.
"Unyonyeshaji wa maziwa ya mama ni miongoni mwa haki za msingi za binadamu ambayo inapaswa kuheshimiwa,kulindwa na kutekelezwa kikamilifu,iwapo watoto watanyonyeshwa ipasavyo maziwa ya mama vifo vitapungua kwa kiwango cha asilimia 13% ambayo ni kiwango kikubwa kuliko afua zote za kupunguza vifo vya watoto" amesisitiza
Maadhimisho haya yanafanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba kwenye vituo vyote vya kutolea huduma za afya,kwa kutoa elimu na unasihi kuhusu unyonyeshaji unaofaa na ulishaji sahihi wa watoto wachanga na wadogo kwa ajili ya maendeleo na ukuaji wa kiakili na kimwili.
Kaulimbiu ya Maadhimisho ya Mwaka 2024 inasema "Tatua changamoto, Saidia unyonyeshaji kwa watoto"
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa