Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Washiriki 63 wa mafunzo ya kampeni ya usajili na utoaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya miaka mitano wametakiwa kutekeleza kampeni hiyo kwa weledi na uadilifu ili kukamilisha zoezi hilo kwa wakati
Ameyasema hayo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji ndg Aloyce Masau wakati akifungua mafunzo ya siku moja kwa wasajili 63 ambao watafanya kampeni hiyo katika maeneo yote ya Wilaya katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Tandahimba
“Kampeni hii ni muhimu sana wajibu wenu ni kufanya kazi hii kwa uadiilifu ili tuweze kufikia lengo la kuwasajili watoto ambao hawana vyeti vya kuzaliwa katika maeneo yetu kwa wakati ambao umepangwa ,”amesema ndg Masau
Aidha amesema kuwa matarajio ya Halmashauri ya Tandahimba ni kuweza kutatua changamoto zilizojitokeza katika kipindi cha awamu ya kwanza ili kuweza kufikia lengo la asilimia 100 katika awamu hii ya pili ya kampeni
Naye mwezeshaji kutoka wakala wa usajili,ufilisi na udhamini (RITA)makao makuu Fakihi Msuya amesema zoezi hilo litafanyika kwa njia ya mfumo hivyo washiriki wahakakikishe wanaingiza taaraifa kwa usahihi
Mafunzo hayo ya siku moja yametolewa kwa watendajiwa wa kata na watoa huduma za afya ngazi za kata, siku nne za zitatumika kuwasajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya miaka mitano zoezi hilo linatekelezwa na serikali na UNICEF
Kampeni ya kuandikisha itaanza tarehe 22-26 June,2021 katika maeneo mbalimbali ya Wilaya,zoezi hili lilifanyika awamu ya kwanza Sept 2017 Halmashauri ya Tandahimba ilipata asilimia 97 kwenye usajili na utoaji w avyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya miaka mitano
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa