Na Kitengo cha Mawasiliano
Mwakilishi kutoka Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara Robert Misungwi ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba kwa ukusanyaji wa Mapato katika kipindi Cha Robo mbili ambapo Wilaya hiyo imekusanya Shilingi Bilioni 5.43 sawa na 97.7% ya Makisio ya makusanyo ya Mapato ya ndani ambayo ni Bilioni 5.56 kutoka katika vyanzo mbalimbali.
Misungwi ameyasema hayo katika Kikao Cha Baraza la Madiwani robo ya pili kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri hiyo na kuongeza kuwa pamoja na ukusanyaji huo waendelee kutumia mashine za kieletroniki (POS) kukusanyia Mapato katika vyanzo mbalimbali kwa kuwa ndio Mfumo rasmi wa Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri.
Akisoma taarifa ya utekelezaji ya kipindi Cha Mwezi Oktoba-Desemba 2023, Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji, Afisa Mipango wa Halmashauri hiyo Charles Mihayo amesema jumla ya Tsh. Bilioni 3.61 zimepokelewa kutoka Serikali kuu ikiwa ni sehemu ya Ruzuku ya Miradi ya Maendeleo na wafadhili.
"Sehemu kubwa ya Fedha hizi ni kwa ajili ya Elimu Bure katika Shule za Halmashauri, fedha za TASAF pamoja na ununuzi wa Vifaa vya kufundishia Katika Shule za Msingi 22". Mihayo
Hata hivyo Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba wameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita Chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha nyingi katika kutekeleza Miradi ya Maendeleo Sekta mbalimbali ikiwemo Afya, Elimu, Maji, Miundombinu ya barabara ambapo kupitia kuimarisha Sekta hizo zimesaidia Wananchi kujikwamua kiuchumi.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa