Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe.Kanali Patrick Sawala ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Kwa kupata hati safi sambamba na kusimamia vyema Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa katika Wilaya hiyo akiwasisitiza kuendelea na ikibidi kuongeza Kasi zaidi .
Kanali Sawala ameyasema hayo Katika Mkutano wa Baraza Maalumu la Madiwani la kujadili hoja za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali 2022/2023.
" Nawapongeza kwa kupata safi, maana yake Kuna watu wamefanya kazi kwa kufuata taratibu, kanuni na Miongozo lakini Hongereni Madiwani Kwa kusimamia tuendelee kushikilia hapo hapo ili tuendelee kupata hati safi"Kanali Sawala
Sambamba na hilo Kanali Sawala amesisitiza kuzuia hoja kabla hazijatokea.
" Tuwe wa kwanza kuzuia hoja, tusiwe mabingwa wa Kujibu hoja,na tunazuia hoja kwa kufuata kanuni, taratibu na Sheria zilizowekwa"
Awali akisoma taarifa ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Mwaka 2022/2023 Mwakilishi wa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Geofrey Mwambalaswa amesema Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba ilipatata hati safi .
Akitoa Salamu Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Michael Mntenjele amesema pamoja na kupata hati safi amewasisitiza Watumishi kuendelea kufanya kazi kwa weledi ili Wilaya hiyo iendelee kupata hati safi.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa