Na Kitengo cha Mawasiliano
Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba imeanza maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji kwa kutoa elimu ya umuhimu wa unyonyeshaji kwa kina mama, wajawazito na akina baba wanaohudhuria kliniki za mama na mtoto katika vituo vya kutolea huduma ya afya
Akizungumza na akina mama ,wajawazito na akina baba ambao wamehudhuria katika kliniki ya mama na mtoto hospitali ya Wilaya ya Tandahimba Agosti 1,2022 Mratibu wa Lishe Dkt Joselyne Kalikawe amewasistiza mtoto wa chini ya miezi sita ya mwanzo kupewa ziwa la mama pekee
Amesema kuwa baadhi ya akina mama wanawapa watoto chini ya miezi sita maji na chakula hiyo hatakiwi,maziwa ya mama yana makundi yote ya chakula lakini maziwa ya mama ya na kinga ya kumzuia mtoto na maradhi mbalimbali pia yanaongeza upendo kati ya mama na mtoto
“Unyonyeshaji unahitajika kwa kiasi kikubwa katika miezi sita ya mwanzo ili kuepuka udumavu na utapiamlo,ukimpa mtoto vyakula vingine unaweza kumsababishia madhara ya kiafya ,”amesema Mratibu
Maadhimisho ya wiki ya Unyonyeshaji Duniani hufanyika kila mwaka ambapo kauli mbiu ya mwaka 2022 “Chukua hatua,Endeleza unyonyeshaji Elimisha na toa msaada”
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa