Na Kitengo cha Habari na Mawasailiano
Mkuu wa Wilaya yaTandahimba Mhe Kanali Patrick Sawala amesema kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa mtu atakayemdhalilisha na kufanya vitendo vya kikatili kwa wanawake
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala akisoma hotuba yake kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake Kiwilaya
Ameyasema hayo kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake Kiwilaya ambayo yamefanyika katika kijiji cha Likolombe kata ya Mkwiti ambapo kauli mbiu ya mwaka huu 2022 ni ‘Kizazi cha usawa kwa maendeleo endelevu’
Wanawake wakifurahia siku yao kwa kucheza
“Tutakuwa wakali na tutachukua hatua kali sanakwa mtu ambaye atabainika amedhalilisha na kumfanyia vitendo vya kikatili mwanamke,lakini mjitokeze kugombea nafasi za uongozi kwa nafasi mbalimbali,hii kaulimbiu isibaki kwenye makaratasi bali itoe matokeo chanya, zingatieni kutimiza wajibu wenu ili muweze kudai haki ”amesema Dc Sawala
Aidha ameeleza kuwa pamoja na wingi wa wanawake kwenye jamii isibaki kwenye namba bali iwe chachu ya kuleta maendeleo na kukataa kuishi kinyonge kwenye dimbwi la umaskini kwa kufanya kazi kwa bidii katika shughuli zinazowaongezea kipato
Dc Sawala akiwa katika viwanja vya maadhimisho hayo ambapo huduma za uchangiaji damu na utoaji wa elimu na chanjo ya Uviko – 19 ilikuwepo aliongoza wananchi kuchangia damu na kueleza kuwa lengo ni kuwasaidia wenye mahitaji hususan mama na mtoto
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Ndugu Mussa Gama amesema kuwa changamoto ambazo wamezibainisha ikiwemo ujenzi wa bweni la wasichana kwa sekondari ya Mkwiti watalifanyia kazi kwa haraka ili wanafunzi wa kike waweze kukaa shuleni
“Changamoto ya bweni nimeichukua na nimeona umbali uliopo tutalifanyia kazi haraka ili wanafunzi wetu wakae bweni ili wapate muda wa kujisomea ni matumaini yangu kuongeza ufaulu wa wanafunzi wetu,”amesema Mkurugenzi
Aidha katika maadhimisho hayo asasi kama vile Shirika la wanawake wenye uthubutu Tandahimba (WAO),Benki ya wananchi wa Tandahimba (TACOBA) Chama kikuu cha Ushirika tawi la Tandahimba(TANECU)Mbunge waJimbo la Tandahimba Mhe.Katani Katani ,Idara ya maendeleo na Shirika la maendeleo ya michezo mashuleni (SDA) wamechangia taulo za kike kwa wanafunzi ,fedha kwa ajili ya kumsaidia mtoto mlemavu anayehitaji kiti mwendo, bima za afya za ICHF kwa familia zinazoongozwa na akina mama sambamba na kuwafungulia wanafunzi 10 akaunti ya Tacoba
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa