Pichani: Mkurugenzi Mtendaji (W) Tandahimba akiwa na maboksi ya POS zilizotolewa na Ofisi ya Rais Tamisemi
Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Tandahimba Said Msomoka amekabidhi mashine 43 za kukusanyia mapato (Point of Sales) kwa ajili ya kuongeza mapato ndani ya Halmashauri
Mkurugenzi Mtendaji wilaya ya Tandahimba (Kulia) akikabidhi POS kwa Mweka Hazina (Kushoto)
Akikabidhi Mashine hizo kwa Mweka hazina wa Halmashauri wilaya ya Tandahimba Ally Machela leo ofisini kwake, alisema mashine hizo zimetolewa na Tamisemi kwa halmashauri kwa ajili ya kukusanyia mapato na zimeunganishwa moja kwa moja na Tamisemi.
“Nakukabidhi mashine hizi ambazo nami nimekabidhiwa na Tamisemi,hivyo naamini zitakwenda kufanya kazi vizuri katika maeneo yetu na mapato yetu yataongezeka kwakuwa zilizopo ukiongeza na hizi zitatusaidia kuongeza mapato katika Halmashauri yetu na hizi zipo kisasa zaidi endapo hautaweka vifurushi kwa wakati inaweza kukuzuia kuendelea kutoa huduma,”alisema Msomoka
Naye Mweka hazina Machela baada ya makabidhiano hayo alisema anashukuru Tamisemi kwa kuwapatia vifaa vya kukusanyia mapato hivyo anatarajia mapato hayo yatakwenda kuongezeka kutokana na mashine hizo ambazo hadi sasa zitakuwa zinafikia 96.
“Tunaishukuru Wizara ya Tamisemi kwa mashine hizi nasi tunakwenda kuzifanyia kazi ili mapato yetu yaongezeke ndani ya Halmashauri yetu,”alisema Machela
Mweka Hazina wilaya ya Tandahimba akitoa neno la shukrani kwa Tamisemi mbele ya Mkurugenzi wilaya ya Tandahimba
Pichani: Mkurugenzi Mtendaji, Saidi Msomoka akiiangalia kwa makini POS
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa