Na Kitengo cha Mawasiliano
Ikiwa imebaki siku moja wanawake kuadhimisha siku ya Wanawake duniani Machi 8,2023 Benki ya Wananchi Tandahimba (TACOBA) imetoa elimu ya kifedha kwa wanawake ili waweze kukuza biashara zao na uchumi wao
Akifungua mafunzo kwa vikundi vya wanawake Machi 6,2023 Meneja Mkuu wa TACOBA Wilaya ya Tandahimba Yahaya Kiyabo amesema kwamba mafunzo hayo ni kukumbushana ili wanawake kuweza kufikia malengo yao sambamba na kutunza kumbukumbu ya hesabu za kila siku katika biashara zao
Kwa upande Mratibu wa dawati la Jinsia Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Bi.Neema Shungu ametoa wito kwa wanawake wa vikundi walioshiriki kuzingatia mafunzo hayo ili yaweze kuwasaidia katika shughuli zao
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa