Taasisi za kidini Wilayani Tandahimba zinatajwa kuwa na ushirikiano Mzuri kwa Serikali katika masuala mbalimbali ya kijamii ikiwemo Elimu, Afya, maji na udumishaji wa Wilaya hali inayochochea ustawi wa Wananchi.
Hayo yameelezwa leo Januari 28, 2024 na Francis Mkuti ambae amemuwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo katika Tamasha la Kwaya za Mtakakatifu Don Bosco Kata ya Luagala .
Aidha, katika hotuba yake Mkuti amewasisitiza Viongozi wa Dini kuendelea kuwahimiza wazazi kuwapeleka watoto wao Shuleni waweze kupata haki yao ya Elimu.
Sambamba na hilo vikundi vya Kwaya vifanye shughuli za Ujasiriamali ikiwemo ufugaji na Kilimo ili viweze kujikwamua kiuchumi.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa