Na Kitengo cha Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala amewasisitiza viongozi na wataalamu kutilia Mkazo na kutoa Elimu ya Umuhimu wa wanafunzi kwenda Shuleni na kuepuka Utoro huku akisistiza kesi za Utoro kushughulikiwa kwa uzito.
DC Sawala ameyasema hayo leo Agosti 16, 2023 kwenye Kikao Cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya(DCC) kilicofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ambapo Taarifa za Idara na vitengo za Halmashauri,RUWASA,TRA,NIDA,TANESCO,TANECU,TARURA,TFS na MAKONDE ziliwasilishwa na kujadiliwa na wajumbe
"Hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wazazi wa mwanafunzi mtoro ili tujenge Jamii yenye Elimu Bora lakini pia viongozi wa Dini mkiwa katika nyumba za ibada endeleeni kujenga uelewa kwa wananchi juu ya umuhimu wa Elimu ," amesema DC Sawala
Kwa upande wao wajumbe wameshauri kuwa Mfuko wa Elimu wa Wilaya ugharamie utengenezaji wa madawati kwa shule zote za msingi ambazo zina upungufu mkubwa wa madawati,upatikanaji wa chakula shuleni uwe ni lazima si hiari na Ofisi ya Mkurugenzi isimamie na kuimarisha vyanzo vya mapato ya ndani
Aidha Wataalamu walipokea ushauri uliotolewa na wajumbe katika kikao hicho na kuahidi kuchua hatua za utekelezaji kwa kuzingatia taratibu na sheria
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa