Na Kitengo cha Mawasiliano
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe.Kanali Ahmed Abbas Ahmed ameisistiza Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba kusimamia bajeti yake kikamilifu na kuhakikisha malengo yaliyojiwekea ya ukusanyaji yanatimia sambamba na kufanya tathimini ya vyanzo vya mapato vilivyopo
Amesema hayo Juni 23,2023 katika Mkutano maalum wa Baraza la Madiwani wa kupitia taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ambapo amesistiza kuwa jukumu la kusimamia miradi ya maendeleo ni la wote lakini wakati wa kusimamia gharama za matumizi yapunguzwe ili mradi ukamilike kwa ubora unaotakiwa
" Halmashauri msimamie bajeti yenu ili miradi ya maendeleo itekelezeke,lakini pia mfanye tathimini ya vyanzo vyenu vya mapato kama mnaona kuna vyanzo vinahitaji kuboreshwa mfanye hivyo ili miradi inayotakiwa kutekelezwa na fedha za mapato ya ndani itekelezwe,msisubiri hadi mpate fedha yote, inapopatikana mnatekeleza yale ambayo mmepanga kutekeleza mwisho mnafikia malengo," amesema RC Ahmed
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa