Shirika lisilo la kiserikali linaloitwa SPORTS DEVELOPMENT AID, kupitia mradi unaoitwa Empowered Girls Speak Out (EGSO) wenye lengo kuwawezesha wanafunzi wenye umri 14- 19 kujitambua, kujiamini, kufikia usawa wa kielimu, kimichezo na kuepukana na changamoto ambazo ni kikwazo kufikia ndoto zao .
Katika Kikao hicho wadau hao wamejadili tathimini ya uelimishaji kwa Jamii na kuona Mafanikio yaliyofikiwa tangu kuanza kwa mradi huo sambamba na Changamoto zilizojitokeza ili waweze kufanya vizuri zaidi.
Pamoja na Elimu hiyo Shirika hilo la SDA limeandaa tamasha la uelimishaji juu ya Jamii kupinga ukatili wa kijinsia, talaka holela sambamba na umuhimu wa malezi Bora.
Washiriki wa kikao hicho kimehusisha wadau mbalimbali wakiwemo Afisa Maendeleo, Ustawi, Utamaduni, watendaji kata, Polisi dawati la jinsia, walimu, wanafunzi, viongozi wa dini, makungwi, walemavu na vijana.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa