Na.Kitengo cha Mawasiliano
Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Wilaya ya Tadahimba wakiongozwa na Mhe.Ismaili Mkadimba wameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita kwa utekelezaji wa mradi wa Maji Makonde wenye thamani ya zaidi yaTsh.Bilioni 84.7 ambao utaongeza upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi.
Pongezi hizo wametoa Oktoba 4,2023 wakiwa kwenye ziara ya ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo ikiwa ni Utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambapo walitembelea mradi huo wa Makonde unaoendelea kutekelezwa Wilaya ya Tandahimba.
Akisoma taarifa ya Utekelezaji wa mradi huo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Makonde Mhandisi Paulusi Nyagali kwa Kamati ya Siasa amesema kuwa kukamilika kwa ujenzi wa mradi wa Makonde utaongeza upatikanaji maji kutoka asilimia 63 iliyopo sasa hadi kufikia asilimia 90 ikiwa ni ongezeko la asilimia 27.
Aidha amesema kuwa mradi wa Makonde utanufaisha Halmashauri nne (4) ambazo ni Tandahimba,Newala Mji,Wilaya ya Newala na Nanyamba zikiwa na wakazi zaidi ya 670,000 ambao umelenga kuongeza uzalishaji maji kwa mita za ujazo 26,000 kwa siku kwa kutumia chanzo cha Maji Mitema ili kukidhi uzalishaji ambapo utakamilika Mwaka wa Fedha 2024/2025
Miradi mingine iliyotembelewa na Kamati ya Siasa siku ya pili ya ziara ni Mradi wa Shule ya Msingi Nandonde, Bweni la Wasichana Shule ya Sekondari Namikupa, ujenzi wa madarasa manne Shule ya Msingi Milidu,Zahanati ya Chikongo,Kituo cha Afya Maheha,Zahanati ya Mnazimmoja,mradi w maji Lipalwe,ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari Mahuta,ujenzi wa Shule ya Sekondari Mndumbwe,Shule ya Msingi Mambamba ujenzi wa nyumba ya mwalimu Shule ya Msingi Machedi na Shule ya Msingi Mjimpya .
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa