na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Serikali imetoa kiasi cha shilingi Bilioni 20 kwa ajili ya kulipa madai ya wakulima wa Korosho kati ya shilingi Bilioni 23 ambayo ilikuwa inadaiwa kwa mwaka 2017/2018
Akikabidhi hundi ya shilingi Bilioni 9 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa kiasi hicho ni deni lote ambalo walikuwa wananadai wakulima wa korosho Wilaya ya Tandahimba
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiongea na wananchama wa amcoss na wananchi wa Wilaya ya Tandahimba
Ameyasema hayo wakati akiongea na wanachama wa chama cha msingi Matogoro na wananchi wa Wilaya ya Tandahimba ,amesema makato kwa wakulima yalikuwa mengi lakini baada ya Rais kupunguza makato sasa mwananchi ananufaika
Wananchi walijitokeza kumsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika viwanja vya ghala la Matogoro Amcoss
“Fedha hizi ni malipo ya madai ya korosho kwa wakulima,lakini malengo yetu tuwe tunaviwanda vya kutosha ili tubangue wenyewe tuzidi kupata zaidi kwakuwa gharama ya korosho ikibanguliwa ni kubwa,”amesema Majaliwa
Aidha Waziri Majaliwa ametoa agizo kwa vyama vya msingi kutoa bei dila kwa zao la korosho katika maeneo husika ili iwe wastani wa Taifa
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (kushoto)akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa
“Zoezi hili la kufanya mahesabu ya wananchi wanatumia kiasi gani kuandaa shamba na wakiuza kiasi gani hawatapata hasara iandikeni kwa maandishi msimu wa mwaka huu tutaanza kuitumia,”amesema Waziri Majaliwa wakati akijibu swali la mwananchi
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa