Na Kitengo cha Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala amesema Serikali itaendelea kuboresha mazingira wezeshi kwa wafanyabiashara kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa biashara katika Wilaya ya Tandahimba
Amesema hayo Septemba 28/2022 wakati akifungua kikao cha baraza la wafanyabiashara Wilaya yaTandahimba katika Ukumbi wa mikutano wa Halimashauri
‘’Serikali inathamini wafanyabiashara na itaendelea kuboresha mazingira wezeshi kwa ajili ya wafanyabiashara lakini pia kupokea ushauri na maoni yenu kwa maendeleo ya Wilaya ya Tandahimba’’ amesema DC Sawala
Aidha amewapongeza wabanguaji wadogo wa korosho wa ndani ya Wilaya kwa kuendelea kuzingatia ubora na kuipa thamani zao la korosho ambapo ilitumia nafasi hiyo kukipongeza kiwanda cha unanguaji cha TDC kilichopo Kata ya Malopokelo kwa kotoa korosho bora na kupata tuzo
Naye Afisa Biashara Ndg Hamisi Natenda akisoma taarifa kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji ambayo imehamasisha wawekezaji kuja kuwekeza Tandahimba ambapo ekari 150 imetengwa katika Kata ya Malopokelo kwa ajili ya uwekezeji wa viwanda vikubwa vya kati na vidogo
Hata hivyo wafanyabiashara walitoa maoni mbalimbali ili kuleta maendeleo katika Wilaya hususani katika biashara ambapo pia walishauri elimu endelevu itolewe kwa wafanyabiashara ili kuwajengea uelewa
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa